
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla
RC Makalla amesema anatambua thamani na mchango wa wazee katika jamii hivyo ameona ni vyema kuanza majukumu yake kwa kukutana nao ili kuchota busara na baraka zao kwani anatambua wazee ni hazina muhimu.
Aidha, RC Makalla amesema katika kutatua kero na changamoto za wananchi amepanga kuanza ziara ya utatuzi wa kero Kata kwa Kata hivyo amewahakikishia wakazi wa Dar es Salaam kuwa anayo dhamira ya dhati kuzipatia majibu kero zao.