Jumatatu , 21st Nov , 2022

Idd Hassan Kimanta aliyewahi kushika nyafidha mbalimbali ikiwemo kuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha ametangazwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Katavi.

Idd Hassan Kimanta, Mwenyekiti mpya wa CCM mkoa wa Katavi

Msimamizi wa uchaguzi wa CCM Wazizi Kidamba amemtangaza Idd Hassan Kimanta kuwa Mwenyekiti mpya wa chama hicho  mkoa baada ya kupata kura 308 dhidi ya mpinzani wake Juma Said Kaombwe aliyepata kura 44.

Akitangaza matokeo hayo mara baada ya uchaguzi huo kumalizika uliofanyika leo Novemba 21, 2022, katika ukumbi wa madini Manispaa ya Mpanda Kidamba amesema idadi ya wajumbe ilikuwa 368 waliopiga kura ni 359 halali 352 zilizoharibika ni 7.

Nafasi ya Mjumbe wa halmashauri kuu CCM Taifa NEC Gilbert Jordan Sampa, ametetea kiti chake baada ya kupata kura 357 akimbwaga chini mgombea mwenza Buhura Chasama aliyepata kura 7 kati ya kura halali 364.

Viongozi hao baada ya kutangazwa wamesisitiza kuimarisha umoja na mshikamamo katika chama wakidai kuwa hawatasita kuwachukulia hatua wanachama watakaoleta  makundi yenye nia ovu.