Ijumaa , 23rd Jun , 2023

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera ametangaza dau la milioni tano kwa yeyote atakaye fanikisha kupatikana kwa mwanafuunzi wa kidato cha tano Ester Noah Mwanyilu wa shule ya Sekondari ya Pandahill aliyetoweka shuleni Mei 18/2023

Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya waziri Mkuu Kasimu Majaliwa kuiagiza ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kufuatilia sakata la kupotea kwa Mwanafunzi huyo

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Joseph Kusaga amesema juhudi za kumtafuta zinaendelea ikiwa ni pamoja na kuwahoji wale wote aliwataja kwenye ujumbe aliocha kabla ya kuondoka 

Mkuu wa shule ya sekondari ya Pandahill Brother Zephania Lusanika amesema kuwa mwanafunzi huyo aliacha ujumbe altareni na kwamba moja ya sababu zilizofanya washindwe kuelewa namna alivyo ondoka ni kutokana  na kamera CCTV kuzimwa kupisha zoezi la mitihani ya Taifa ya kidato cha sita mwaka huu