Alhamisi , 26th Mei , 2022

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla ameamuru kusimamia kwa Shughuli zote za uchimbaji wa madini kwenye eneo la mwekezaji Boko lililovamiwa huku akitoa wiki moja kwa Wavamizi kuondoa mali na kokoto walizochimba Mara moja.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla

RC Makalla ametoa maelekezo hayo alipotembelea eneo Hilo lenye ukubwa wa hekta 70 ambapo tayari Mahakama ilishatoa haki kwa Kiwanda Cha Al Hushiim Investment ltd ambao ndio mmiliki halali.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo alipotembelea eneo Hilo lenye ukubwa wa hekta 70 ambapo tayari Mahakama ilishatoa haki kwa Kiwanda Cha Al Hushiim Investment ltd ambao ndio mmiliki halali.

Aidha RC Makalla amesema eneo Hilo ni mahususi kwaajili ya Shughuli za uchimbaji wa madini ambapo amepiga marufuku eneo kutumika Kama Makazi na kuelekeza kuanza kwa mchakato wa Kiwanda Cha saruji.

Hata hivyo RC Makalla ameelekeza Jeshi la Polisi kuanza doria ya kulinda eneo Hilo kwa kushirikiana na walinzi wa kampuni hiyo ambapo amesema Magari yatakayoruhusiwa kuingia ni Yale yanayokwenda kuchukuwa mzigo pekee na sio uchimbaji.

Pamoja na hayo RC Makalla amemuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Godwin Gondwe kufika kwenye eneo baada siku Saba kuanzia leo ili kujirudhisha.