
Dk. Shein ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam, alipotembelea maonyesha ya biashara ya Kimataifa Sabasaba na kuwataka wajasiriamali kuwa wabunifu kulingana na mahitaji yaliyopo kwenye jamii.
Aidha, Dk. Shein amewataka watanzania kujenga tabia ya kutumia na kuthamini bidhaa zinazotengenezwa na wazalishaji wa ndani kwani bidhaa nyingi hazina tofauti na zizalishwaji nchini.
Mbali na kusifia ubora wa bidhaa za mwaka huu katika maonyesho hayo Dk. Shein amesema, kwa upande wa Zanzibar tayari walishaanza harakati za kuwepo na viwanda kwa miaka 5 iliyopita licha spidi ya uhitaji wa viwanda hivyo kutoendana na uchumi uliyopo.