Ijumaa , 30th Sep , 2022

Rais wa zamani wa Zambia Edgar Lungu , amesema kwamba yupo tayari kukumbana na mkono wa sheria endapo aliiba wakati wa utawala wake.

  Lungu alipoteza kiti cha Urais kwenye uchanguzi mkuu mwaka jana.

 Bw.Lungu amesema kwamba hafurahishwi na tuhuma za yeye pamoja na viongozi wengine waandaamizi wa serikali iliyopita wakichunguzwa kwa jinai ambazo walifanya wakati wa utawala wake. 

Kiongozi huyo wa zamani amesema kwamba hakupendezwa na kitendo cha wachunguzi kuelekea kwenye shamba lake siku ya jana na kuanza uchunguzi wao. 

BwLungu ametaka ikiwezekana Rais Hakainde Hichilema kumuondolea kinga ya kutoshtakiwa kikatib aili afikishwe mahakamani kusafisha jina lake

  Lungu alipoteza kiti cha Urais mwaka jana baada ya kushindwa na Rais Hichilema, amekua akinanusha shutuma mbaolimbali za rushwa kipindi cha utawala wake.