Jumatano , 12th Jan , 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo Januari 12, 2022, amekutana na kuzungumza na aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai Ikulu ya Chamwino Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa na Mhe. Job Ndugai

Rais Samia amekutana na Mheshimiwa Ndugai, zikiwa zimepita siku 6 tu tangu aandike barua yake ya kujiuzulu kwa hiari yake mwenyewe nafasi ya Uspika wa Bunge, huku akisema ameamua kufanya hivyo ili kulinda maslahi mapana ya Taifa, serikali na chama chake.