Ijumaa , 13th Jun , 2025

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufani, George Mcheche Masaju kuwa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania akichukua nafasi ya Prof. Ibrahim Hamis Juma ambaye amestaafu.

Uapisho wa Jaji Mkuu utafanyika June 15, 2025 Ikulu, Chamwino Dodoma kuanzia saa 4.00 asubuhi.

April 20,2023 Rais Samia alimteua Jaji George Masaju kuwa Mshauri wa Rais, Masuala ya Sheria (Advisor to the President - Legal Affairs) wakati huo Jaji Masaju alikuwa ni Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma.

Baadaye January 10,2025 Rais Samia akafanya uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya Rufani wanne akiwemo Jaji George Mcheche Masaju ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu na Mshauri wa Rais, Sheria.