Ijumaa , 10th Jun , 2016

Rais Barack Obama wa Marekani amemuidhinisha rasmi, Bi. Hillary Clinton, kuwa mgombea urais wa Marekani aliyeteuliwa na Chama cha Democratic.

Uamuzi huo wa rais Obama, umekuja baada ya kukutana na muwania urais mwingine wa chama hicho Seneta Bernie Sanders ambaye amekuwa akichuana na Bi. Clinton kuwania uteuzi.

Akimuongelea mgombea huyo kupitia twitti ya video, rais Obama amesema Bi. Clinton anaweza kuwa moja ya mtu mwenye sifa zaidi na vigezo ambaye hajawahi kutokea kuwania wadhifa wa urais katika miaka nyuma.