Jumatatu , 25th Jul , 2016

Leo ni siku ya maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kukumbuka wale wote walipoteza maisha wakati wakipigania haki ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Jordan Rugimbana akiongea na baadhi wa viongozi wa serikali waliohudhuria tukio hilo la uwashwaji wa Mwenge

Maandhimisho hayo yamezinduliwa rasmi kwa kuwashwa kwa mwenge wa Uhuru, katika uwanja ambao utatumika kwa sherehe hizo huko mjini Dodoma hii leo ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Akizungumza mara baada ya kuwashwa kwa mwenge huo waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, kazi, vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema maadhimisho hayo yanapaswa kuwakumbusha watanzania kuwa Wazalendo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana ameishukuru serikali kuyafanyia maadhimisho hayo mkoani kwake huku akisema maadhimisho ni muhimu kwa kuwa yanalenga kukumbusha uzalendo wa nchi kwa kila Mtanzania.

Sauti ya waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, kazi, vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama
Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana