Jumapili , 15th Jul , 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga Bw. Fadhili Nkurlu kuanzia leo Julai 15, 2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Kufuatia hatua hiyo, Rais Magufuli amemteua Bw. Anamringi Macha kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama. Bw. Anamringi Macha anatakiwa kuripoti katika kituo chake cha kazi mara moja.

Kabla ya uteuzi huo, Macha alikuwa Katibu wa Sekretarieti ya Halmashauri ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)