Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwaongoza waombolezaji kuaga mwili wa Marehemu Joseph Muungai katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam Novemba 10,2016
Shughuli za kuuaga mwili marehemu Mungai zimefanyika katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na vyama vya siasa.
Akiwasilisha salam za serikali, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga amesema, serikali inatambua mchango wa marehemu Mungai kwa kiwango kikubwa ambacho kimeliwezesha taifa kufika hapa lilipo hasa katika sekta ya kilimo na elimu.
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akitoa salamu za serikali wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Joseph Muungai katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam Novemba 10,2016
Kwa upande wake mtoto mkubwa wa marehemu, Jimmy Mungai amesema baba yake alikuwa ni nguzo kubwa katika familia yao na hadi mauti inamkuta familia bado ilikuwa inamhitaji kwa kiasi kikubwa.
Kwa upande wake mbunge wa zamani wa Bunda Mjini Steven Wasira amesema viongozi wa Tanzania wana wajibu wa kuiga matendo mema ya marehemu Mungai.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Rais Mstaafu awamu ya tatu Benjamin Mkapa pamoja na waombolezaji wengine walipofika kuaga mwili wa Marehemu Joseph Muungai katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam Novemba 10,2016
Pamoja na Rais Magufuli Viongozi wengine waliofika kuuaga mwili wa Marehemu Mungai ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa, Makamu wa Rais Mstaafu Mhe. Mohamed Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba, Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Frederick Tluway Sumaye, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Viongozi wengine mbalimbali wa Serikali na Siasa.
Marehemu Joseph Mungai ambaye alifariki dunia juzi jioni Jijini Dar es Salaam, utasafirishwa kesho kuelekea Mafinga mkoani Iringa na kuzikwa Jumamosi saa 8 mchana huko Mafinga