Jumatatu , 15th Mei , 2017

Rais Dkt. John Magufuli ameivunja rasmi Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) na kuagiza mali na shughuli zote zilizokuwa zikifanywa na CDA zihamishiwe Halmashauri ya Manispaa Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitia Saini Amri ya Rais kuvunja Mamlaka ya Ustawishaji wa Makao Makuu Dodoma (CDA) Ikulu jijini Dar es salaam

Rais Magufuli amesema uamuazi kwa kuivunja Mamlaka hiyo ni kutokana na kutaka kuhamishia majukumu yake katika Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma ili kuondoa mkanganyiko wa utoaji wa huduma kwa wananchi uliokuwa ukisababishwa na mgongano kati ya vyombo hivyo viwili na pia kuendana na mahitaji ya sasa ambayo yamedhidhirisha kuwa hakuna haja ya kuwepo kwa CDA.