Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais Magufuli amezungumza hayo kwenye shughuli ya upokeaji wa gawio kutoka kwa shirika hilo, shughuli ambayo imefanyika katika ofisi za makao yake makuu jijini Dar es salaam.
"Nakumbuka mwaka jana idadi ya waeja walikuwa milion 1.8 lakini mmeongeza hadi kufikia milioni 2, nawapongeza sana lakini nakurudia wito wangu kwa Watanzania kuwa rudini nyumbani kumenoga", amesema Rais Magufuli.
"Pamoja na kwamba mmefanya mafanikio makubwa, bado mna safari ndefu ili mufikie kuitwa Shirika la Mawasiliano la Taifa, mnafahamu watu wenye simu nchini wanafikia milioni 40 nyinyi mna watu Mil. 2.2 maanake soko lenu ni chini ya asilimia tano hamna budi kuongeza bidii", ameongeza.
"Naomba niletewe orodha ya viongozi ambao wanatumia laini za TTCL na sio ziwepo tu bila kutumika, huwezi kulipwa mshahara wa serikali na hutumii mtandao huo, sijamaanisha msitumie mitandao mingine"- amesema Rais Magufuli.
Katika hafla hiyo Rais Magufuli amepokea gawio la Shilingi bilioni 2 kutoka shirika hilo.