Jumatatu , 11th Jun , 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Fidelis Mutakyamirwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Ushauri wa Ardhi.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Bw. Mutakyamirwa umeanza leo tarehe 11 Juni, 2018.