Jumanne , 8th Apr , 2014

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete ametunukiwa tuzo ya African Most Impactful Leader of the year na taasisi ya uchapishaji ya African Leadership Magazine ya nchini Marekani.

Rais wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete ametunukiwa tuzo ya African Most Impactful Leader of the year na taasisi ya uchapishaji ya African Leadership Magazine ya nchini Marekani.

Tuzo hiyo ya Rais itapokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Benard Membe na atarejea nchini ifikapo April 11 baada ya kupokea Tozo hiyo.

Kwa mujibu wa Taasisi ya African Leadership Magazine, Tuzo hiyo inatolewa kwa Mhe. Rais Kikwete kutokana na namna ya pekee ya uongozi wake wenye matokeo yanayopimika kiutawala bora hususan kwa mwananchi wa kawaida wa Tanzania.

Aidha, uongozi wake umeiletea Tanzania heshima kubwa kimataifa na kuiweka Tanzania kama chaguo muhimu kwa wawekezaji kutokana na ukuaji uchumi na maboresho ya sera.

Tuzo hiyo tayari imewahi kutolewa kwa marais na Viongozi wengine mbalimbali wa Afrika wakiwemo Mhe. Ellen Johnson Sirleaf Rais wa Liberia, Mhe. James Michel Rais wa Shelisheli na Rais Mstaafu wa Ghana Mhe. John Kuffor.