Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania amesema serikali itaendelea kuboresha sekta ya elimu hapa nchini kwa lengo la kuhakikisha vijana wanaosoma katika shule za sekondari wanapata elimu bora mara kabla ya kuhitimu.
Rais Kikwete amesema hayo leo jijini Dar es salaam mara baada ya kupokea vitabu milioni 2 na laki 5 vya masomo ya Sayansi na Hisabati kutoka serikakali ya Marekani kupitia balozi wake hapa nchini Bw. Mark Childress.
Amesema kupitia vitabu hivyo vimesaidia kupunguza uhaba wa vitabu uliokuwepo katika shule za sekodari kutoka uwiano wa watoto watano kusoma kitabu kimoja na kufikia watoto mtoto mmoja kusoma kitabu kimoja kwa sasa.
Aidha Rais Kikwete amezitaka taasisi za serikali kutumia majeshi yaliyopo katika kusafirisha vitu vya serikali kama ilivyofanywa na ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI katika kusafirisha vitabu hivyo na kuvipeleka katika kila mkoa kwa kuwa kufanya hivyo kutaondoa uwezekano wa vitendo vya rushwa iwapo kama tenda hiyo ingetangazwa kwa lengo la kupata mzabuni