Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha ikulu na kufanya mazungumzo na mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia hapa nchini Bwana Philipe Dongier
Viongozi hao walijadili mageuzi yaliyofanyika katika uchumi wa nchi ya Tanzania kwenye vipindi tofauti vikiwemo vya wakati mgumu wa kiuchumi kwa nchi katika miaka ya mwanzoni mwa 1980 hadi sasa.
Aidha Rais Kikwete amemshukuru Dongier kuinua kiwango cha uchumi kwa ushirikiano wa Tanzania na Benki ya Dunia katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo iliyotekelezwa na Benki ya Dunia nchini.
Kwa upande wake Mwakilishi huyo wa benki ya Dunia ameeleza utayari wa benki hiyo kuongeza kasi ya ushirikiano wake na Tanzania katika eneo hilo.