Jumanne , 13th Feb , 2024

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema amewahi kufanya kazi na  Hayati Edward Lowassa kwa vipindi tofauti katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya awamu ya tatu na awamu ya nne .

Amesema taarifa ya msiba huu ameipokea kwa masikitiko makubwa, pia anatoa pole kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wananchi wote wa Zanzibar. 

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipofika nyumbani kwa Waziri Mkuu wa zamani  Hayati Edward Lowassa akiwa na Mama Mariam Mwinyi na kuifariji familia yake akiwemo Mama Regina Lowassa na wana familia wote Masaki Jijini Dar es Salaam tarehe: 12 Februari 2024.