Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulrahman Kinana.
Kinana ameyasema hayo leo Julai 26, 2023 wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mkendo Musoma Mjini, mkoani Mara.
"Nataka niwahakikishie msiamini kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyekula kiapo eti atafanya jambo ambalo halina maslahi na nchi, haiwezi kutokea, Rais ambaye tangu amechukua usukani amefanya mambo mengi mazuri, kwanini aende kuuza bandari, sababu ni ipi?" amesema Kinana
Aidha Kinana ameongeza kuwa "Ili apate nini, ili iweje na ukisikiliza huu mjadala usikilizeni kwa makini na mmeshausikiliza, wote tunaoutetea, wanaopinga pamoja na wanaokosoa hakuna anayesema kwamba kusiwe na uwekezaji hata mmoja kwani wote wanakubali kwamba kuna haja ya kuwekeza na lengo ni moja tu kuongeza ufanisi na kuongeza mapato,".
Katika hatua nyingine Kinana ameongeza kuwa, "Serikali imesema tunakwenda kufanya kazi hii kwa nia njema ya kuongeza ufanisi, kuongeza mapato tuweze kufanya shughuli nyngi zaidi za maendeleo. Wamejitokeza watu wameanza kuhoji, wako wanaohoji kwa nia njema ya kujenga ya uzalendo, hatuwezi kusema kila anayehoji anania mbaya,"