Jumapili , 23rd Jul , 2023

Waziri wa Elimu Profesa Adolf Mkenda, ameonya tabia ya vitendo vya unyanyasaji wa wanafunzi katika baadhi ya vyuo nchini ambapo amebainisha kuwa serikali haitasita kuchukua hatua za kisheria kwa watakaobainika kufanya vitendo hivyo.

Waziri wa Elimu Profesa Adolf Mkenda,

Aidha amewataka wakuu wa vyuo hivyo kutekeleza muongozo wa ulinzi na usalama wa wanafunzi wanapokuwa vyuoni.

Prof.Mkenda ameyasema hayo katika uzinduzi wa muongozo wa ulinzi na usalama wa wanafunzi wa vyuo vya maendeleo ya wananchi na vyuo vya elimu na mafunzo ya ufundi stadi, ulioandaliwa na jumuiya ya vyuo na Taasisi za Canada.