Jumapili , 1st Feb , 2015

Chama cha Wananchi CUF kimewataka wananchi kutowachukia polisi kufuatia kitendo cha kutotenda haki kwa raia ikiwemo kuwabambikizia kesi mbalimbali na kuwashushia vipigo bila sababu zozote.

Profesa Ibrahim Lipumba

Hayo yalisemwa na mwenyekiti wa taifa wa chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo Profesa Lipumba amesema ameanza kufanya utaratibu wa kuonana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete ili kumuelezea udhaifu uliopo katika jeshi la polisi ili nchi isije kuingia kwenye matatizo kati ya jeshi la polisi na wananchi.

Pia Prof Lipumba ameishauri serikali kuzifanyia marekebisho baadhi ya sheria zinazosababisha uadui kati ya polisi na raia, ikiwemo sheria ya jeshi la polisi pamoja na ya uchaguzi na kuangalia uwezekano wa kubadili mfumo wa kiutendaji wa jeshi hilo