Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira jiji la Arusha ,James Lobikoki
Wananchi hao wakizungumza katika operesheni ya tokomeza kipindupindu iliyoendeshwa na Ofisi ya Mkuu wa wilaya kwa kushirikiana na Halmashauri na kamati ya Ulinzi na usalama wameteketeza mitambo ya kupikia pombe hizo aina ya piwa, dadi na chang`aa ambazo pia huathiri afya za watu.
Ester Stephano Shaka ambaye ni Muuzaji wa pombe hizo na Wilfred Lyakimu na wamesema kuwa maisha yao yanategemea biashara ya pombe za kienyeji ambazo huwasaidia kusomesha watoto na kupata mahitaji ya nyumbani hivyo ameiomba serikali iwapatie mikopo ili waweze kufanya biashara mbadala badala ya kutumia nguvu kutokomeza biashara hiyo.
Mkazi wa Matejo Jovan George amesema kuwa kutokana na tatizo la ajira limewapelekea watu wengi kujiingiza katika biashara hiyo na matumizi ya pombe hivyo ameitaka serikali kutafuta njia mbadala.
Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira jiji la Arusha ,James Lobikoki amesema kuwa uteketezaji wa pombe haramu ni moja kati ya jitihada wanazozifanya katika utekelezaji wa operesheni tokomeza kwani kutokana na mazingira machafu ya uandaaji wa pombe hizo kwani zoezi hilo ni endelevu.
Ugonjwa wa kipindupindu umeenea katika maeneo mengi nchini tayari wananchi wameanza kuchukua tahadhari ya kuweka mazingira safi licha ya baadhi ya maeneo kukithiri kwa uchafu hivyo kukwamisha jitihada za kutokomeza ugonjwa huo.