
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Jumanne Muliro,
Akiongea na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Jumanne Muliro, amesema watuhumiwa hao wamekamatwa kufuatia ufuatiliaji mkubwa wa wahalifu wanao jihusisha na matukio ya namna hiyo.
Aidha Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linaendelea na ufuatiliaji wa wahalifu wanaopora kwa kutumia pikipiki katika maeneo mbalimbali ya jiji, na jeshi la polisi litawakamata na baadae kuwafikisha katika vyombo vingine vya kisheria kwa hatua zaidi.