
Hayo yameelezwa na Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Ahmed Msangi wakati alipokuwa anazungumzia juu ya tukio hilo na kusema kwamba mnamo Juni 09, 2018 majira ya saa 5:00 usiku katika mtaa wa Misungwi ambapo kikundi cha walinzi walimkamata mwananchi ambaye alifahamika jina la Christian Audock Joseph wakiwa wanamtuhumu kwa kosa la wizi katika maduka waliyokuwa wanayalinda.
Msikilize hapa chini Kamanda Ahmed Msangi akielezea tukio zima jinsi lilivyotokea mpaka muuguzi huyo kufariki dunia na kupelekea askari wa Jeshi la Polisi kutuhumiwa na mauaji hayo.