Waandishi hao walikuwa wakifanya kazi zao za kujulisha ulimwengu kinachoendelea nchini humo na vibali vyao vimesitishwa.
Waandishi hao ni Philipe Remy mwenye asili ya Ufaransa, mwandishi wa habari wa gazeti la Le Monde la Ufaransa pamoja na Phil Moore mpiga picha raia wa Uingereza walikamatwa na polisi katika kata ya Nyakabiga katikati ya jiji la Bujumbura wakiwa na vitambulisho halali vinavyowapa ruhusa ya kufanya kazi ya uandishi wa habari nchini humo.
Hata hivyo hii ni mara ya kwanza kwa waandishi wa habari wa kimataifa kukamatwa na polisi tangu mgogoro ulipoanza mwezi wa Aprili, 2014 baada ya Rais Pierre Nkurunzinza kutangaza kugombea muhula wa tatu.
Aidha Polisi wamewatuhumu waandishi hao kushirikiana na makundi ya watu ambao polisi inawatuhumu kuwa ni wahalifu.
Chanzo VOA


