Jumatatu , 26th Aug , 2024

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imeteketeza jumla ya ekari 1,165 za mashamba ya bangi na kukamata kilogramu 102 za mbegu za bangi ikiwa ni matokeo ya oparesheni maalum Mkoani Morogoro iliyofanyika kwa siku tisa 

Imefanyika katika vijiji vya Nyarutanga, Lujenge na Mafumbo vilivyopo Wilaya za Morogoro vijijini na Kilosa ambapo katika vijiji vya Mafumbo na Lujenge

Katika oparesheni iliyofanyika kijiji cha Nyarutanga Watu 6 wakiwa na kilogramu 342 za bangi wamekamatwa na watafikishwa Mahakamani taratibu za kisheria zitakapokamilika.

Akiongea baada ya uteketezaji wa mashamba hayo, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo amesema, mashamba ya bangi yaliyoteketezwa yamelimwa pembezoni mwa Mto Mbakana, Misigiri na Mgeta kwenye eneo la akiba la Hifadhi ya Taifa Mikumi.

Lyimo amewashukuru sana Wananchi hususan Vijana waliojitolea kushiriki katika zoezi zima la uteketezaji wa mashamba ya bangi pamoja na Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha Mamlaka kuweza kufanya operesheni za kuteketeza mashamba ya bangi na kutokomeza dawa za kulevya Tanzania