
Pichani wafuasi wa CHADEMA.
Kamanda Mkonda amekanusha taarifa hizo leo Septemba 28, baada ya kuwepo kwa uvumi kuwa msafara wa Tundu Lissu umeshambuliwa na mabomu eneo la Nyamongo wakati wakielekea wilayani Serengeti.
Aidha Kamanda Mkonda amesemakuwa mabomu yalipigwa ili kutawanya wafuasi amabao walikuwa wakishamabulia askari wa jeshi hilo.
Taarifa ya CHADEMA mapema leo ilidai kuwa polisi wenye silaha kali wamevamia msafara wa mgombea wa Urais Mhe. Tundu Lissu Nyamongo, mkoani Mara na wamepiga mabomu ya machozi na kujeruhi watu.