Jumatano , 21st Sep , 2022

Jeshi la Polisi Kitengo cha usalama barabarani limeahidi kuwa litaeendelea kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara, huku akiwapongeza wadau kutoka sekta binasfi ambao wamekuwa wakitoa elimu ya usalama barabarani.

Askari wa usalama barabarani akimsaidia mwananchi kuvuka barabara

Hayo yameelezwa na Mrakibu Msaidizi wa Polisi Notker Kilewa ambaye ni  Kaimu Mkuu wa usalama barabarani Mkoa wa Kinondoni akihimiza kuwa wataendelea kulinda usalama wa raia na mali zao, na hasa watumiaji wa vyombo vya moto.

Aidha Kamanda Notker amewakumbusha wananchi kuendelea kutii sheria za usalama barabarani bila shuruti, ili kupunguza ajali na usumbufu barabarani.