
Polisi nchini Zimbabwe wakiwatawanya waandamanaji wanaopinga hali mbaya ya uchumi.
Chama cha Movement for Democratic Change kimetoa malalamiko kwamba polisi wamewatia mbaroni wafuasi wake licha ya amri ya mahakama kuruhusu maandamano hayo kuendelea.
Kumekuwa na maandamano katika miezi ya hivi karibuni nchini humo dhidi ya serikali ya Rais Robert Mugabe kutokana na kudorora kwa uchumi na kuanzishwa kwa mipango ya noti mpya.