Jumapili , 27th Jul , 2014

Jeshi la polisi nchini Tanzania limesema limeimarisha hali ya ulinzi katika maeneo yote ya nchi katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu ya Eid El Fitri.

Msemaji wa Polisi SSP Advera Bulimba.

Msemaji wa jeshi hilo Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Advera Bulimba, amesema jeshi hilo limejipanga kuhakikisha wananchi wanasheherekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu huku akiwataka wazazi kuwa waangalifu na watoto wanapokuwa katika maeneo yaliyo jirani na fukwe za bahari.

Aidha SSP Bulimba amewataka wananchi wachukue tahadhari za kiusalama kwani uzoefu unaonesha kuwa baadhi ya watu hutumia kipindi hicho cha sikukuu kama mwanya wa kufanya matukio ya uhalifu kutokana na kuwepo kwa mikusanyiko mikubwa ya watu.