Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu
IGP Mangu ameyasema hayo walipokutana na Kamati ya kudumu ya Bunge kwa malengo yakujua namna jeshi hilo linavyotumia fedha zilizoidhinishwa katika bajeti ya kwa ajili ya shughuli za Jeshi hilo
Amesema wana mpango wakuanza kufanya maboresho wa Jeshi la Polisi kwa nchi nzima kwa kutumia rasilimali wanazopata kwa kuhakikisha pesa wanazokusanya kwa tozo mbalimbali za makosa zinarudisha huduma kwa jamii ya watanzania na kuhakikisha inaongeza ulinzi hasa maeneo ya mipakani na kuondoa usumbufu wa uhalifu hadi kwenye mitaa mbalimbali nchini.
Katika hatua nyingine IGP Mangu ameongeza kuwa wananchi waache kujichukilia sheria mikononi kwa kuwapiga watu ovyo kwani wengine sio wahalifu kama wanavyowadhania na hivyo kupelekea vifo au majeruhi kwa wasio na hatia.
Kwa upande wake Mwenyekiti msaidizi wa kamati za kudumu za bunge za hesabu za serikali PAC Aesh Hillary amesema Jeshi la Polisi litolee maelezo mkataba wa jeshi hilo walioingia na mkandarasi wa kampuni ya Lugumi yakufunga mitambo maalum ya ukaguzi yenye thamani ya Shilingi Bilion 34 Tanzania nzima kwani mitambo hiyo bado haijafungwa na pesa za serikali tayari zimetolewa kumlipa mkandarasi hiyo.