Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli(katika)Kulia kwake ni Mkuu wa jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu na (kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba)
Rais Magufuli amesema hayo leo Jijini Dar es Salaam, wakati wa Hafla ya kula kiapo cha maadili kwa watumishi wa umma kwa ambapo leo Makamishna wa jeshi la Polisi walioteuliwa hivi karibuni walikuwa wanatekeleza zoezi hilo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli amesema kuwa alipinga uwepo wa Polisi jamii tangu akiwa waziri wa Uvuvi na kusema kwa sasa ni lazima ifike mahala raia atakapokutana na polisi amuogope kwa kuwa dunia ya sasa imebadilika na raia abaki kuwa raia na Polisi abaki na nafasi yake.
Amiri Jeshi Mkuu amewataka Polisi kuchukua hatua za kisheria kukabiliana na watu wanaovamia vituo vya Polisi ambao wanahatarisha maisha yao na sio kudai ni Polisi jamii wakati wanavunja sheria.
Lakini Mhe Rais amesisitiza polisi hao wanavochukua hatua dhisi ya wahalifu hao wazingatie sheria ili wasionee watu wema ambao wanafata sheria za nchi kama katiba ya nchi inavyosema.
Aidha amewaahidi kulinda maslahi ya jeshi hilo na kuwawekea mazingira mazuri ya kufanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuwaongeza mishahara pamoja na kuwapandisha vyeo kwa wale ambao wataonekana kufanya vizuri zaidi.









