
Picha ya Bastola ikiwa na risasi
Kulingana na ripoti iliyoandikishwa kituoni hapo Alhamisi, Juni 20,2019 Obiri alikuwa amepoteza fahamu na hakuweza kuzungumza wakati alikimbizwa katika hospitali ya Avenue ili kufanyiwa uchunguzi wa matibabu.
"Maafisa wa polisi waliomtembelea walimpata akiwa amelazwa baada ya kupelekwa hospitalini humo akiwa hali mahututi na maafisa wa polisi wa Parklands. Afisa huyo alipewa dawa aina ya opioid kulingana na uchunguzi wa madaktari," imesema ripoti hiyo.
Bastola yake iliyochukuliwa ilikuwa na risasi 14. Hata hivyo hii sio mara ya kwanza kwa maafisa wa polisi kupoteza silaha zao mikononi mwa wahalifu nchini humo.
Jumanne, Aprili 16, majambazi walivamia kituo cha polisi kaunti ya Nandi na kuiba bunduki tatu wakati maafisa waliokuwa wakishika doria walikuwa wameenda kutazama mechi.