
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,CP Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam
Akizungumza jana Jijini Dar es Salama Kamishana wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam Suleiman Kova ambapo ametoa ripoti ya kukamatwa kwa watuhumiwa wengine watatu wa tukio la uvamizi la kituo cha Staki shari akiwemo mtuhumiwa mmoja aliyejisalimisha polisi akiwa na wake zake.
Kamanda Kova amesema jeshi hilo limeunda kikosi maalumu cha kusimamia vituo vya polisi kwa kuimarisha ulinzi huku wakiendelea na opresheni hiyo ya kuwasaka watuhumiwa huku akisema watuhumiwa waliokamatwa hivi karibuni bado wanahojiwa na jeshi hilo.
Aidha Kamnda Kova ameongeza kuwa vikundu hivyo vya uhalifu ambavyo wakati mwingine vinapata fedha kwa kuvamia taasisi za fedha vyote vimeundiwa vikosi ili kuweza kukomesha kabisa wizi wa kwenye taaasisi hizo hasa kwenye Mabenki.
Kamanda Kova aliwataja waliokamatwa katika operesheni hiyo ni pamoja na Bw. Zahak Rashid Ngai ambae alijisalimisha mwenyewe polisi akiwa na wake zake mwingine ni Ramadhani Hamis pamoja na kijana mwingine aliejukana kwa jina la Omary Omary Ally na kufanya idadi ya waliokamtwa kuhusiana na tukio hilo kufikia 8 ambapo watatu kati ya hao walifariki katika tukio la ukamataji.