Waziri wa Viwanda na Biashara nchini Tanzania, Mhe. Charles Mwijage,
Akiongea mara baada ya kumpokea waziri wa viwanda na biashara wa Oman, Al Maoud Al Sunaid, amesema ujio huo ni muendelezo wa mahusiano baina ya nchi mbili ambapo kati ya sehemu watakazoangazia ni kuongeza thamani ya mazao na ukanda huru wa uwekezaji.
Mhe. Mwijage amesema Falsafa ya Tanzania kwa sasa ni kutokuuza nje ya nchi mazao ghafi na badala yake serikali imejipanga kuzalisha zaidi kuchakata mazao kwa kuongeza thamani ili yaende Moja kwa moja sokoni.
Aidha Mhe Mwijage amesema watatumia fursa hiyo kutoka kwa wafabiashara hao ambao wanafani mbalimbali kuweza kukuza sekta ya kilimo pamoja na uwekezaji ili kufikia malengo endelevu kupitia sekta ya viwanda na biashara nchini.