Jumanne , 20th Jan , 2015

Wafugaji 266 wa kijiji cha Mabwegere  wilayani Kilosa mkoani Morogoro hawana makazi baada ya nyumba zao  kuchomwa moto na wakulima.

Nyumba hizo zimechomwa moto baada ya kuzuka kwa mgogoro wa ardhi ambapo  nyumba 38 zimeteketea kabisa na mazao ya chakula  kuharibiwa huku baadhi ya wanawake  na watoto wakilazimika kukimbilia kanisani kuomba hifadhi.

Wakizungumza kwa uchungu wanawake hao na watoto wamelalamikia baadhi yao  kubakwa na kufanyiwa ukatili na wengine hadi sasa  hawajulikani walipo ambapo wameeleza  kupata hasara kubwa  ya kuchomewa nyumba zao   huku wakiiomba serikali kutizama upya mgogoro huo   wa wakulima na wafugaji  ili haki itendeke kwani mgogoro huo unawaumiza  wanawake na watoto.

EATV imetembelea maeneo ya nyumba zilizochomwa moto na kukuta baadhi ya nyumba zikiendelea kuungua  huku vyakula navyo vikiteketea  kwa  moto ambapo mwenyekiti wa kijiji na baadhi ya wamiliki wa nyumba hizo  wamesema chanzo cha mgogoro  ni  wakulima kuingia kwa nguvu  katika mashamba ya kijiji cha wafugaji.

Baadhi ya vijana wa kimasai yaani morani wameonekana msituni wakiwa na silaha za jadi ambapo wamesema wanawasaka wakulima waliohusika na tukio hilo na  kuendelea kulinda mipaka ya kijiji kuzuia wakulimawasiingie kwa nguvu.

Jeshi la polsi mkoa wa morogoro limethibitisha kutokea  kwa tukio hilo na askari wameonekana wakiwa na silaha wakiimarisha ulinzi   katika kijiji cha Mabwegere