Jumanne , 3rd Nov , 2015

Wafanyabiashara wa Nyama ya ng'ombe katika manispaa ya Dodoma wametangaza kupandisha bei ya nyama kutoka elfu 6000 hadi elfu 7000 huku jijini Dar es Salaam ikipanda kutoka 6000 mpaka 8000 na sehemu nyingine ikifika hadi elfu 10000.

Nyama ikiwa bushani tayari kwa kuuzwa kwa mlaji wa kawaida

Wakiongea kwa nyakati tofauti Mjini Dodoma na Jijini Dar es Salaam Wauzaji wa Kitoweo hicho wamesema kuwa hali hiyo inakuja baada ya kuadimika kwa Ng'ombe kwa kiasi kikubwa.

Aidha kwa upande wake mwenyekiti wa wauza nyama mjini Dodoma amefafanua kuwa hali hiyo inatokana na kupanda kwa bei ya ng'ombe kwa kuwa wameadimika kutokana na ukame unaokabili maeneo mbalimbali nchini Tanzania.

Naye meneja uzalishaji wa machinjio ya kisasa mjini humo Khamis Kissoi amesema kuna tatizo la upatikanaji wa ng'ombe na kwa sasa wamekuwa wakipokea nchini ya ng'ombe 180 kwa siku tofauti na hapo awali.