Menyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa Njombe Deo Sanga ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Njombe Kaskazini
Ombi hilo limetolewa wakati wa kampeni za ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuomba ridhaa kwa wanachama kumpigia kura mbunge atakaye shindanishwa na wabunge wa vyama vingine mwezi Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi mkuu.
Wananchi wa kata za Maguvani, Makambako, Mwembetogwa na Majengo wameomba wagombea wawili walio wania jimbo hilo kuteuliwa na wanachama kuwakilisha chama hicho akiwemo mbunge wa jimbo la Njombe Kaskazini Deo Sanga ambaye kwa sasa amechukua fomu ya jimbo jipya la Makambako ambalo limegawika kutika jimbo la Njombe kaskazini akiwa na mgombea mwenzeka Alimwimike Essau.
Mmoja wa wakazi wa kata ya Majengo Hamis Mhagama akiuliza swali kwa wagombea amesema kuwa CCM imekuwa kwa mda mrefu madarakani lakini imeshindwa kuwaletea maji katika maeneo yao je wagombea wanawahakikishia vipi kama wakiwachagua watawaletea maji.
Amesema kuwa kila wanapo kuja kuomba kura wanawaambia watawaletea maji na mara ya mwisho kutolewa ahadi ya maji waliwaambia wachimbe mtaro kwa ajili ya maji lakini mtaro ulichimbwa mpaka unajifukia hawana maji.
Akijibu swali la maji kutoka kwa wananchi mbunge Sanga amesema kuwa alitoa agizo la kuletwa kwa mabomba ya maji katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo lakini serikali pesa ili chelewesha ma kufanya mabomba hayo kutofika.
Amesema kuwa akiteuliwa na wanachama hao na kupigiwa kura kuwa mbunge na kuingiza bungeni tena atahakikisha anapigania maji katika jimbo hilo na kuwa alivunja bodi ya maji baada ya kuona haina kazi inaitwa bodi ya maji na maji hakuna.
Akijinaji katika moja ya mikutano Essau alisema kuwa wananchi wasiutegemee pesa za mbunge na kuwaomba wawe tayari kuungamkono juhudi za mbunge na kuwa akiteuliwa na wanachama hao na kuwa mbunge atahakikisha fedha za jimbo zina ingizwa katika mradi wa maji ili kuinua uchumi wa wakazi wa jimbo hilo ambao wanadidimia kutokana na muda mwingi kutumia kutafuta maji.