Ijumaa , 6th Sep , 2024

Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Raymond Mndolwa amewataka wakandarasi wanaojenga mradi wa umwagiliaji skimu ya Mkombazi Mkoani Iringa kuongeza kasi ujenzi wa miradi hiyo ili kuhakikisha uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali unanufaisha wakulima katika msimu ujao.

Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Raymond Mndolwa

Amewataka wakandarasi hao kuwa na mkakati wa kumaliza ujenzi wa miradi hiyo hadi kufikia mwishoni mwa Oktoba mwaka huu

Akizungumza katika vikao kazi baina ya uongozi wa Tume na wakandarasi hao mkaoni humo Mndolwa amesisitiza wakandarasi hao wafanye kazi usiku na mchana kumaliza mradi kwa wakati.

Wakandarasi wanaojenga mradi wa Mkombozi lot I na lot II unaofanywa na kampuni ya ndani ya Cimfix & engineering, sambamba na ujenzi wa mradi Mkombozi lot III na lot IV unajengwa na kampuni ya CRJE Engineering kutoka China

Mndolwa pia aliongoza  kikao kazi baina ya Tume  na Mkandarasi ujenzi wa Mkombozi M/S Cimfix& Engineering Co Ltd kilicho fanyika katika kambi ya Mkandarasi anayetekeleza  mradi wa Mkombozi lot I na II Mkoani Iringa.