Jumanne , 11th Apr , 2017

Mbunge wa Sumbawanga Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) , Aeshi Hilaly amefunguka na kusema alitishwa na mmoja wa kiongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam hivyo saizi yeye anaogopa kukanyaga mkoa huo.

Mbunge wa Sumbawanga Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) , Aeshi Hilaly.

Mbunge Aeshi amesema hayo leo Bungeni na kusema wakati kiongozi huyo akimtisha alikuwepo na Mkuu wa Wilaya Kinondoni Mhe. Ally Hapi 

"Kuna kitu ambacho kinaniuma naomba leo nikiseme mimi ni miongoni mwa watu ambao nilitishwa, tena mimi sikutishwa kwa maneno nimemuona yeye mwenyewe nimekutana naye uso kwa uso, akiniambia kwamba wabunge mmezidi unafiki kwa ubaya zaidi maneno haya ameyatamka mbele ya Mkuu wa Wilaya Kinondoni. Akisema kwamba wabunge mmezidi unafiki na nitadili na nyinyi nikianza na wewe, mimi leo Mhe. Dar es Salaama sikanyagi na naiogopa yaani nilikuwa nimei miss mno lakini baada ya kutishwa nimeogopa imebidi nikae Dodoma na Sumbawanga" alisema Aeshi 

Mbunge huyo anasema ameamua kusema hivyo ili bunge liweze kujua pia familia yake iweze kujua kuwa na yeye ni miongoni mwa watu ambao wametishwa na moja ya kiongozi wa mkoa wa Dar es Salaam.