Jumapili , 8th Mar , 2020

Mtangazaji wa muda mrefu Betty Mkwasa, ambaye pia ni Mke wa Kocha Msaidizi wa timu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa, amesema kuwa alipoanza kazi ya utangazaji yeye alizidi kuwa maarufu zaidi kuliko mume wake.

Betty Mkwasa na Mume wake Charles Mkwasa

Hayo ameyabainisha leo Machi 8, 2020, katika kipindi maalum cha Mwanamke Kinara, kilichoruka mubashara kupita EATV&EA Radio pamoja na mitandao yake ya kijamii, ikiwa ni maadhimisho ya kusherehekea siku ya Kimataifa ya wanawake duniani, inayoadhimishwa duniani kote.

"Nilianza kuishi na Charles Mkwasa mwaka 1985 na ndoa tukafunga mwaka 1989, kipindi hicho yeye alikuwa ni supa staa wa Yanga, lakini baadaye mimi nikaja kuwa supa staa na yeye akawa wa kawaida" amesema Betty Mkwasa.

Aidha Betty Mkwasa ameeleza nia yake ya kuendelea na utangazaji kwa ajili ya kulinda jina lake lisife.