Jumatano , 21st Sep , 2022

Tume ya Taifa ya uchaguzi nchini Nigeria imeyathibitisha majina 18 ya wagombea Urais nchini humo katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi  February mwakani.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye tume hiyo ya uchaguzi (INEC) imesema kwamba vyama vya siasa 18 viliwateua wagombea wake na manaibu wagombea Urais. 

 Moja ya majina makubwa yaliyomo  ni lile la mwanasiasa mkongwe nchini humo mwenye umri wa miaka 75 ambaye ni makamu wa zamani wa Rais nchini humo Atiku Abubakar kutoka chama pinzani cha Peoples' Democratic Party,  akiwemo pia gavana wa zamani wa  jiji la Lagos Bw.Ahmed Bola Tinubu,mwenye umri wa miaka 70  wa chama tawala cha cha All Progressives Congress.

Ukosefu mkubwa wa usalama, ukosefu wa ajira na uchumi mbaya vinatarajiwa kuwa ajenda kubwa kwenye uchaguzi huo ujao. Nigeria ina watu zaidi ya milioni 200 ambapo watu milioni 95    wameshajiandikisha kupiga kura nchini humo. 

Kampeni za uchaguzi zinatarajiwa kuanza kuridnima jumatano wiki ijayo