Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Ni yeye Mheshimiwa Hamisi Mwinjuma "Mwana Fa"

Ijumaa , 30th Oct , 2020

Msanii Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana Fa amefanikiwa kushinda nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Muheza,Tanga kupitia Chama Cha Mapinduzi 'CCM' akimshinda mpinzani wake Yosepher Komba wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo 'CHADEMA'.

Msanii na Mbunge wa Jimbo la Muheza Mwana Fa

Kwa mujibu wa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Muheza, amemtangaza Mwana Fa wa CCM kuwa ndiye mshindi wa nafasi ya ubunge wa Jimbo hilo baada ya kupata kura 47,578 na kumshinda Yosepher Komba wa CHADEMA aliyepata kura 12,034.

Mwana Fa anaungana na wasanii wengine ambao waliingia Bungeni kama Joseph Mbilinyi aliyeshindwa kutetea nafasi yake ya Ubunge Jimbo la Mbeya Mjini na Joseph Haule 'Prof Jay' aliyeshindwa nafasi ya Ubunge Jimbo la Mikumi.

Watu wengi wamempongeza Mwana Fa kwa matokeo hayo akiwemo mtu wake wa karibu na msanii AY ambaye kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika kuwa "Ni Mheshimiwa Hamisi Mwinjuma 'Mwana Fa' kwenye moja na mbili hongera,  hatimae ndoto yako ya muda mrefu ya kuwatumikia ndugu zako wa Muheza, kila la kheri mwanangu maana nakuaminia kwenye mipango ya kimaendeleo, Mungu ni mwema sana sasa kazi ianze

HABARI ZAIDI

Mbunge wa Kilosa Profesa Palamagamba Kabudi

"Ndege ijayo ipewe jina la Mwl Nyerere" - Profesa

Baadhi ya Wanachi wa Kata ya Msowero, wakiwa Katika Mkutano wa Hadhara na Mkuu wa Wilaya

Mwenyekiti atiwa mbaroni kwa kuuza mlima, Msowero

Sehemu iliyokumbwa na Mafuriko Kusini mwa Brazil

Wanaokufa kutokana na mafuriko waongezeka Brazil

Baadhi ya Wabunge Wakichangia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Uchukuzi

Serikali yashauriwa kuwa bunifu sekta ya usafiri

Baadhi ya Wananchi Wakishudia Ajali Iliyomgonga Mwendesha Bodaboda

Watatu wanusurika kifo, scania ikimgonga bodaboda

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Deogratius Ndejembi (kulia) pamoja na Meneja Mwandamizi wa Afya, Usalama na Mazingira kutoka GGML, Dk Kiva Mvungi (kushoto) wakimpatia vifaa kinga mmoja wa washiriki wa mafunzo kwa madereva bodaboda wa jiji la Arusha.

Bodaboda 200 Jijini Arusha wanolewa na kufundwa