Mwenyekiti wa NEC Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage
Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa NEC Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage ambapo amefafanua kuwa hatua hiyo inajiri baada ya kukamilisha mchakato wa Uteuzi wa majina ya wagombea wa vyama mbalimbali vya siasa kwa nafasi ya Urais hii leo.
"Leo tumeanza kuzisikiliza Rufaa zilizowasilishwa na wagombea waliokata kutoka majimbo mara baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya awali, baada ya kusikiliza tutatoa maamuzi kulingana na sheria na taratibu zilizopo", amesema Jaji Kaijage.
Wakati huo huo Tume imetoa wito kwa makundi mbalimbali kuendelea kuheshimu sheria za uchaguzi zilizowekwa ili kuhakikisha kila raia mwenye haki ya kupiga kura wanatimiza wajibu wao kikatiba.