Ijumaa , 7th Jan , 2022

Katibu wa Bunge amesema baada ya Job Ndugai kujiuzulu, kwa sasa taratibu za uchaguzi kwa ajili ya kujaza nafasi hiyo zinaendelea ambapo kamati zilizokuwa zikutane kuanzia Januari 10 na Januari 17 sasa zitakutana Februari Mosi hadi 11 wakati wa mkutano wa sita wa Bunge.

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taarifa hiyo ya Katibu imetolewa leo Januari 7, 2022, na kusema kutokana na hali hiyo wabunge watatakiwa kufika bungeni Januari 31, 2022.

Job Ndugai alijiuzulu wadhifa wake hapo jana kwa kusema amefanya hivyo kwa hiari yake na kwa kulinda maslahi mapana ya Taifa, serikali na chama chake.