Alhamisi , 1st Dec , 2016

Muungano wa nchi zionazozalisha mafuta kwa wingi duniani (OPEC) zimekubali kupunguza uzalishaji wa mafuta hatua ambayo ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka nane ili kuimarisha bei ya mafuta duniani.

Mohammed Bin Saleh Al-Sada - Rais wa OPEC

 

Rais wa OPEC Mohammed Bin Saleh Al-Sada, amesema punguzo la mapipa milioni 1.2 kwa siku litaanza kuanzia mwezi Januari mwakani hatua ambayo inafuatia kushuka kwa bei ya mafuta kulikodumu kwa miaka miwili.

Kufuatia hatua hiyo ya OPEC ya kupunguza uzalishaji wa mafuta, nchi zinazozalisha mafuta ambazo siyo mwanachama wa OPEC nazo zinatarajiwa kupunguza uzalishaji kwa mapipa 600,000 kwa siku  kulingana na taarifa iliyotolewa na Rais wa Opec Al-Sada.