Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara la EAC Prf. Mayunga Nkunya
Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Felexs Mosha amesema jitihada za kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana wakiwemo wanaomaliza vyuo vikuu zitakuwa na mafanikio kama serikali za nchi wanachama zitakubali kuwa na mfumo shirikishi wa elimu na unaozingatia mahitaji soko la ajira kwa sasa.
Bw Mosha ameyasema hayo katika mkutano wa Baraza hilo la biashara na Baraza la Vyuo Vikuu la Afrika Mashariki, Baraza la Biashara la Afrika Mashariki na Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki, unaofanyika Kigali, nchini Rwanda..
Katibu Mtendaji wa baraza hilo Prf. Mayunga Nkunya amesema pamoja na changamoto zinazowakabili wahitimu wa vyuo vikuu katika nchi za Afrika Mashariki uchumguzi umeonesha kuwa wana uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko kama mfumo uliopo utabadilika.
Akizungumza wakati anafungua mkutano huo waziri wa elimu wa Rwanda Prof. Silas Lwakabamba amesema licha ya vyuo vikuu vya EAC kuzalisha wahitimu wanaokubalika katika soko la ajira hawauziki kutokana na kuwa na kujengwa katika mfumo usiokidhi soko la ajira la sasa