Jumatatu , 4th Jan , 2016

Taasisi ya utafiti ya kimataifa(IAA) kwa kushirikiana na watafiti wa zao la mhogo kutoka vituo vya utafiti vya Naliendele, Kibaha,Hombolo,Makutupora na Zanzibar wameanza utafiti unaoshirikisha sampuli za mbegu zilizozalishwa upya maabara

mtafiti msaidizi kutoka taasisi ya utafiti wa kilimo na maendeleo ya Naliendele Mtwara,Ignas Gambo

Hayo yamebainshwa katika kituo cha utafiti cha Makutupora mkoani Dodoma,ambapo mbegu hizo zimepandwa zikiwa tayari kusambazwa kwenye mashamba ya vituo vya utafiti ili kuangalia ubora wake kabla ya kukaguliwa na wakala wa udhibiti wa ubora wa mbegu na zitakazoonekana bora zaidi zisambazwe kwa wakulima,

Akiziungumza na kituo hiki mtafiti msaidizi kutoka taasisi ya utafiti wa kilimo na maendeleo ya Naliendele Mtwara,Ignas Gambo,amesema enewo hilo la makutupora wamepanda aina 30 za mbegu,baada ya kuzitengeneza upya maabara,zikiwa ni sampuli kutoka nchi za Tanzanzia,Kenya,Uganda,Malawi na Msumbiji,

Kwa upande wake mtafiti wa mhogo kanda ya kati,Elizabeth Mpango amesema utafiti huo utaendelea kwà mwaka mzima ili kupata mbegu bora zaidi.

Nae mratibu wa utafiti wa zao la muhogo Kitaifa Dkt. Godfrey Mkamilo amesema kutokana na changamoto kubwa ya magonjwa katika mazao ya mihogo ikiwemo michirizi ya kahawia na Batobato wameamua kushirikiana na nchi hizo tano kupata mbegu bora itakayo tumika kwenye nchi hizo na kwamba waliangalia mbegu bora kutoka nchi hizo zenye uwezo wa kuzalisha zaidi tofauti na mbegu zingine.