
Naibu Waziri Ulega amefikia uamuzi huo wakati wa ziara yake aliyoifanya jijini Mwanza iliyokuwa imelenga kabainisha sababu za kukithiri kwa biashara ya Samaki waliovuliwa kinyume cha sheria.
Ulega amechukua uamuzi huo baada ya kubaini maafisa hao kushindwa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi ambapo wanadaiwa kutoa vibali vya kusafirisha Samaki waliovuliwa kinyume na sheria.
Aidha Naibu Waziri amesema maafisa hao wameikosesha mapato serikali huku akiwataka wafanyabiashara wanaonunua Samaki katika soko hilo kuwa wazalendo kwa kulinda rasilimali za nchi.
Idadi ya Samaki waliokamatwa wiki hii katika soko la kimataifa la Kirumba imefikia tani 11, Samaki hao walikuwa wamepakiwa tayari kwa kusafirishwa kwenda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).